̽»¨¾«Ñ¡

Jinsi COVID-19 ilivyoathiri SDG katika Afrika

Get monthly
e-newsletter

Jinsi COVID-19 ilivyoathiri SDG katika Afrika

Ripoti ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2021 inabainisha hatua muhimu, lakini janga tandavu limekuwa pigo kuu.
Afrika Upya: 
18 July 2021
Bi. Yongyi Min
UN Photo
Bi. Yongyi Min, Mkuu wa Sehemu ya Ufuatiliaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu katika Kitengo cha Takwimu cha Idara ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kiuchumi na Kijamii.
Ikiwa huwezi kusoma sasa, sikiliza tu toleo la sauti: 
Sauti ya Kiingereza

Kwa miongo miwili iliyopita, Afrika imepiga hatua kubwa katika maeneo mbalimbali ya maendeleo. Kumekuwa na punguo katika vifo vya kina mama watoto, punguo thabiti katika viwango vya Ukimwi, malaria na kifua kikuu, hatua muhimu katika usajili wa wanafunzi katika shule za msingi na viwango vya kusoma na kuandika, na kuimarika kwa ushiriki wa wanawake katika siasa.Ìý

Hata hivyo, kanda hii pia inakabiliwa na changamoto kuu, ikiwa ni pamoja na ongezeko la kasi la idadi ya watu, viwango vya juu vya umaskini na njaa, na mizozo ya silaha, ambayo kwa jumla inaleta ugumu katika kutekeleza Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya 2030 ambayo ni pana na muhimu katika kanda hii.

Tangu mwezi Machi 2020, janga la COVID-19 limesababisha uharibifu mkubwa kwa maisha ya watu na vitekauchumi vyao ulimwenguni kote.ÌýÌýIngawaje viwango vya maambukizi ya COVID-19 katika Afrika haviko juu kama katika maeneo mengine, kuzorota kwa uchumi na kutatizwa kwa mfumo wa kijamii kulikosababishwa na janga hili kunaharibu maendeleo muhimu yaliyopatikana kwa miongo mingi katika bara hili.

Makala haya yanafichua baadhi ya athari za kusikitisha za janga hili katika utekelezwaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SGD) katika Afrika huku yakitumia data na makadirio ya hivi karibuni kabisa kutoka ripoti iliyotolewa hivi karibuni ya ÌýnaÌýthe .

COVID-19 imesababisha uharibifu wa hali ya juu wa vitekauchumi katika Afrika

SDG 1Ìý– Kiwango cha watu wanaoishi katika umaskini mkuu katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara kilipungua kutoka 59% mwaka 2000 hadi 41% mwaka 2018, lakini maendeleo yalikuwa yamesita tangu 2015.Ìý

Kwa sababu ya ukuaji wa kasi wa idadi ya watu, idadi ya walio maskini kabisa katika eneo hili imeongezek katika miongo miwili iliyopita, hadi kwa takriban milioni 439 mwaka wa 2019, ambayo ni zaidi ya thuluthi tatu ya watu maskini zaidi ulimwenguni. Ìý

Ingawaje idadi ya watu maskini ilikuwa imekadiriwa kuongezeka tayari mwaka 2020 na 2021, janga la COVID-19 linakadiriwa kuongeza viwango hivi vya kushangaza maradufu na kuwasukuma watu milioni 30 zaidi katika umaskini mkuu katika kanda hii.

Idadi ya watu wanaoishi chini ya $1.90 kwa siku katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara, 2015-2021, (mamilioni)

SDG 2Ìý– Hata kabla ya janga hili, idadi ya watu waliokuwa wakiumia kutokana na njaa na ukosefu wa utoshelevu wa chankula ilikuwa ikiongezeka katika Afrika tangu 2014. COVID-19 inasukuma idadi hii juu zaidi.

Mwaka 2020, mtu mmoja kati ya watano alikuwa akikabiliwa na njaa katika Afrika, takriban watu milioni 46 zaidi ikilinganishwa na 2019. Karibu 60% ya watu wa Afrika—watu milioni 799—waliathiriwa na ukosefu wa utoshelevu kadri au wa juu wa chakula mwaka 2020.

Wiano na idadi ya watu wanaokabiliwa na utapiamlo katika Afrika, 2015–2020 (asilimia na mamilioni)

SDG 3Ìý–ÌýKatika miongo miwili iliyopita, Afrika imepiga hatua muhimu katika maeneo mengi ya afya, ikiwa ni pamoja na kuimarisha afya ya kina mama na watoto, na kukabiliana na Ukimwi, malaria, na kifua kiku (TB). Kwa mfano, maambukizi ya ukimwi kati ya watu wazima (miaka 15 hadi 49) yalipungua kwa 47% katika Afrika Kusini mwa Sahara kati ya 2010 na 2019.Ìý

Hata hivyo, kanda hii inaendelea kuubeba mzigo mzito zaidi wa kiafya na ina miundomsingi dhaifu zaidi ya afya ulimwenguni. Mwaka wa 2019, kanda hii ilikuwa na 94% ya visa vyote vya malaria (visa milioni 215).

Wiano wa wauguzi na wakunga katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara ni 10 kwa watu 10,000, punguo la thuluthi moja ya ule wa Mataifa ya Kaskazini ya Amerika. Takriban 90% ya mataifa ulimwenguni yanaripoti kuvuruga kwa aina moja au zaidi kwa huduma muhimu za kiafya kwa sababu ya janga hili. Hata kuvuruga kwa wastani tu kupatikana kwa matibabu kunaweza kusababisha vifo vingi. Ìý

Kwa mfano, kuvuruga kwa 10% kupata matibabu kamilifu ya malaria eneo la Afrika Kusini mwa Sahara kunaweza kusababisha vifo 19,000 zaidi katika kanda hii. Katika juma la pili la Julai, Afrika ilisajili 43% ya vifo kutokana na COVID-19 kila juma.

Hata hivyo, kuna ukosefu mkuu wa usawa katika ugavi wa chanjo: kufikia tarehe 17 Juni 2021, takriban chanjo 68 zilitolewa kwa kila watu 100 Ulaya na Mataifa ya Amerika Kaskazini ikilinganishwa na chini ya 2 Afrika kusini mwa Sahara.

Health workers in short supply
COVID-19 has led to health care workers shortage

SDG 4Ìý– Afrika Kusini mwa Sahara ina viwango vya chini kabisa vya ufundishwaji na vya watoto wasio shuleni. Huku kuhitimisha elimu ya msingi kukiongezeka taratibu, kutoka Ìý46% mwaka 2000 hadi 62% 2019, kiwango cha kuhitimisha sekondari kimeongezeka kutoka 18% hadi 25% tu katika kipindi hiki.Ìý

Janga la COVID-19 linakadiriwa kuwafanya watoto milioni 6 zaidi katika madarasa 1-8 katika kanda hii kutotimiza viwango vya usomaji bora, huku likiongeza idadi ya wanafunzi wanaobaki nyuma hadi 85% mwaka 2020. Kufunga shule na kuzorota kwa uchumi kulikosababishwa na COVID-19 kumeongeza vurugu dhidi ya watoto, ajira za watoto, ndoa za watoto, na mimba za mapema.

SDG 5Ìý–Wanawake katika kanda hii wanapata mamlaka zaidi katika siasa. Idadi ya viti vinavyokaliwa na wanawake katika bunge au mabunge ya kitaifa viliongezeka kutoka 18.4% mwaka 2010 hadi 25% 2015. Ufanisi mkuu katika uwakilishi wa wanawake katika miaka 20 iliyopita umekuwa nchini Rwanda, huku 61.3% ya viti vikikaliwa na wanawake katika bunge au bunge la kitaifa.Ìý

Athari za kijamii na kiuchumi za janga la COVID-19 zimekwaza hatua zakutimiza usawa wa kijinsia mno.Ìý

Vurugu dhidi ya wanawake na wasichana imeongezeka; ndoa za watoto zinatarajiwa kuongezeka; na wanawake wamepoteza ajira zaidi na kuongeza huduma za nyumbani.

Unequal vaccine distribution

SDG 7Ìý– Kati ya watu milioni 759 wasio na umeme ulimwenguni mwaka 2019, robo tatu yao wanaishi katika Afrika Kusini mwa Sahara.

Idadi ya watu wasio na umeme Afrika iliongezeka mwaka 2020 baada ya kupungua taratibu tangu 2013, huku ikiyasukuma mataifa mengi mbali na kutimiza lengo la kutoa umeme kwa wote kufikia 2030.

SDG 8Ìý–ÌýAjira zisizo rasmi ziliwakilisha 85% ya ajira zote katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara. Wafanyakazi hawa wameathiriwa sana na kanuni za marufuku ya kutembea, kwa sababu ya ukosefu wa mpango wa kijamii wa kuwaauni watu. ÌýWanakabiliwa na hatari kuu ya kutumbukia katika umaskini na watashuhudia changamoto kuu kurejelea vitekauchumi vyao katika kipindi cha kujikomboa.

Mabadiliko ya tabianchi, kuzorota kwa mazingira, na mizozo inaendelea kukwaza juhudi za maendeleo endelevu

SDG 12-15Ìý– Licha ya kudorora kwa uchumi kunakohusiana na janga hili, hatari ya kimazingira inaendelea bila kusitishwa. Mabadiliko ya tabianchi ni miongoni mwa mambo makuu yanayochangia ongezeko la njaa na uhamisho wa lazima wa watu katika Afrika.

Zaidi ya humusi ya ardhi katika Afrika imeharibika. Zaidi ya 70% ya watu wanaoishi katika Afrika Kusini mwa Sahara wanaitegemea misitu na vichaka kupata riziki, ihali Afrika ilishuhudia kiwango cha juu zaidi cha kuisha kwa misitu kutoka 2010–2020, kwa ekari milioniÌý 3.9.

Uharibifu wa ardhi na mazingira umetishia maendeleo ya Afrika, kudhoofisha hali ya mamilioni ya watu, kusababisha kuisha kabisa kwa baadhi ya spishi (nusu ya ndege na mamalia wamo katika hatari ya kuisha kufikia mwisho wa 2100); na kuongeza kasi ya mabadiliko ya tabianchi.

SDG 16Ìý– Mizozo kati ya mataifa na makundi yaliyojihami, na mashambulizi dhidi ya raia yanaendelea kuongezeka katika maeneo mengi ya eneo la Afrika Kusini mwa Sahara.

Bila shaka, hatari ya COVID-19 inakwaza utimizwaji wa SDG. Hata hivyo, hatari hii inatupa fursa kamili kuweka ramani ya mwelekeo mpya.Ìý

Kati ya 2015 na 2020, vifo vya kila mwaka vya raia ulimwenguni vilipungua kwa 61%, lakini katika eneo la Afrika Kusini mwa Sahara, vifo vya raia kutokana na mizozo viliongezeka kwa 66%.ÌýÌýMataifa ya Afrika Kusini mwa Sahara yana viwango vya juu vya wastani wa hongo.

Kwa wastani, zaidi ya mmoja kati ya watu wanne waliotagusana na maafisa wa serikali katika kanda hii walitoa hongo au walitakiwa kutoa hongo. ÌýÌýÌý

Mizozo, ufisadi na COVID-19 inakoleza changamoto za maendeleo kwa mataifa mengi ya Afrika.

Fauka ya yote, Afrika inaweza kujenga upya na vyema kama mwelekeo wa kimageuzi ukichukuliwa

Uwajibikiaji upesi COVID-19 wa Afrika umepongezwa kama kampeni fanifu ya kukabiliana na msambao wa COVID-19. Kufikia tarehe16 Julai 2021, Afrika ilikuwa imesajili takriban vifo 106,000, ikilinganishwa na zaidi ya 1,950,000 katika mataifa ya Amerika na zaidi ya 1,200,000 Uropa. Kati ya tarehe 1 Februari 2020 na 10 Mei 2021, mataifa 51 ya Afrika yalitangaza hatua 238 za ulinzi wa kijamii ili kuwajibikia hatari ya COVID-19, ikiwa ni pamoja na hatua za afyaÌý na utoshelevu wa chakula, ulinzi wa wasio na ajira, ulinzi wa mapato, na marupurupu maalum na ya kodi.

Bila shaka, hatari ya COVID-19 imekwaza utimizwaji wa SDG zaidi. Hata hivyo, hatari hii inatoa fursa kamili kwetu kuweka ramani ya mwelekeo tofauti, mwelekeo ambao unatambua mianya ya kina katika mwelekeo wa sasa na unaojumuisha masuluhisho ya kukabiliana na hatari sambamba za kimazingira, kijamii na za kiuchumi. ÌýSDG na Mkataba wa Makubaliano wa Paris inatupa miongozo. Hatua ya kwanza katika ukombozi na kujenga upya vyema ni kuhakikisha ugavi sawa wa chanjo na matibabu ya COVID-19. Mataifa katika kanda hii yametatizika kupata chanjo. Viwango vya utoaji chanjo vimesalia chini ikilinganishwa na ulimwengu wote, huku chini ya 2% ya idadi ya watu Afrika ikiwa imechanjwa kikamilifu. Ugavi wa chanjo za COVID-19 katikaAfrika umeimarika katika majuma ya hivi karibuni baada ya kukwama kwa zaidi ya miezi miwili.Ìý

Aidha, huku zikitumia ufanisi wa awali na kutumikisha nguvu wenzo za eneo huru la kibiashara kubwa zaidi ulimwenguni, mataifa ya Afrika yanaweza kunyakua fursa ya kufanya mageuzi na uwekezaji utakaokuwa muhimu kwa ukombozi endelevu na maendeleo endelevu kwa kipindi kirefu kwa kasi.


Bi. Yongyi Min ni Mkuu wa Kitengo cha Uangalizi wa Mlengo ya Maendeleo Endelevu katika Idara ya Uchumi na Maendeleo ya Kijamii ya Divisheni ya Takwimu (UN DESA) ya Umoja wa Mataifa.

More from this author