̽»¨¾«Ñ¡

Hoteli inayoelea ya Crabshack inastawi juu ya miti ya mikoko

Get monthly
e-newsletter

Hoteli inayoelea ya Crabshack inastawi juu ya miti ya mikoko

Wakati wa msimu wa wageni wengi hoteli hii hupata wateja 1,000 kwa siku na mapato ya kila mwezi hufika dola 30,000 na kuajiri wafanyakazi 42.
Afrika Upya: 
23 January 2023
Dabaso Mangrove floating restaurant.
Haji Abdikarim
Dabaso Mangrove floating restaurant.

Mnamo mwaka wa 2008, Dickson Mazinga alikuwa mpishi mkuu katika hoteli moja ya kifahari katika mji wa Watamu ulio pwani ya Kenya. Aliacha kazi yake na kujiunga na vijana kutoka kijiji cha Dabaso nje kidogo ya Watamu kulinda msitu wa mikoko.ÌýMsitu huo ulikuwa unaangamia kutokana na ukataji wa magogo ya kutumiwa katika ujenzi wa nyumba.

Hivi sasa Bw. Mazinga anamiliki hoteli ambayo inaning’inia juu ya miti ya mikoko, miti ambayo ni maarufu sana kwa kufyonza hewa chafu ya kaboni kwa kulinganishwa na miti mingine yote duniani.ÌýHoteli hiyo imeboresha misitu kwa kiasi kikubwa, pamoja na maisha yake na maisha ya wengine wengi.

Bw. Mazinga ni mmoja wa waanzilishi wa kikundi cha vijana 47 wa kujitolea katika kijiji cha Dabaso ambao walihofia uharibifu wa msitu wa mikoko uliokuwa umeshamiri kwenye ufuo wa bahari ya Hindi. Walijitolea kuelimisha wanakijiji kuhusu jukumu muhimu la mikoko katika kutoa makazi kwa viumbe wa baharini, haswa katika hatua za kuzaa na kulea.

"Tulifanya kazi kwa kujitolea kwa kipindi cha miaka saba," anasema Bw. Mazinga. “Kisha baadhi ya washirika wetu kutoka Taasisi ya Utafiti wa Majini na Uvuvi ya Kenya (KMFRI) walituomba tuanzishe mradi ambao ungeleta mapato. Walithamini kazi yetu na matokeo yake mazuri. Hawakutaka kuhatarisha kupotea kwa wanachama kama wakienda kutafuta kazi ya kuwapa mapato kwingine.

Walishangazw na jinsi wenyeji walipenda nyama ya kaa. Ugunduzi huu uliwafanya wanachama kujaribu kufungua hoteli yao wenyewe. Kupitia uzoefu wao na kufanya kazi na wamiliki wengine wa biashara ya hoteli, walikuwa na uhakika kwamba wangeweza kufungua na kuendesha hoteli ambayo ingewaletea faida - na hivyo ndivyo walivyofanya.

KAMFRI ilionyesha watu waliojitolea jinsi kaa wanavyozaliana chini ya mikoko. Bw. Mazinga anasema kuwa kikundi chake kilishangaa kujua ni aina ngapi za viumbe wa baharini wanaoondoka kwenye bahari kuu na kwenda kujificha mbali na wanyama wanaokula wenzao chini ya miti ya mikoko wakati wa msimu wa kuzaa.

"Wataalamu wa KAMFRI walitufundisha kuvuna kaa wachanga na kuwakuza kwa ajili ya soko," Mazinga anasema. “Walitusaidia kujenga vizimba vinavyofaa chini ya mikoko ili kuanzisha kilimo chetu cha kaa. Mara tu tulipoanza, tulipata soko tayari katika hoteli za mji."

Kenyan coastal villagers are cashing in on carbon credits.
Haji Abdikarim

Bw. Mazinga anaongeza kwamba walishangazwa na jinsi wenyeji walipenda nyama ya kaa. Ugunduzi huu uliwafanya wanachama kujaribu kufungua hoteli yao wenyewe. Kupitia uzoefu wao na kufanya kazi na wamiliki wengine wa biashara ya hoteli, walikuwa na uhakika kwamba wangeweza kufungua na kuendesha hoteli ambayo ingewaletea faida - na hivyo ndivyo walivyofanya.

Wanakikundi waliita hoteli yao Crabshack na kumchagua Bw. Mazinga kama meneja mkuu na katibu mratibu.

Hapo zamani, nilikuwa nikitoka nyumbani saa kumi na moja asubuhi na kurudi nyumbani baada ya saa nne usiku kila siku, na niliishi katika nyumba iliyojengwa kwa udongo. Pia nilihangaika kuwapeleka watoto wangu shule za mitaa. Sasa, ninaishi katika nyumba yangu nzuri iliyojengwa kwa matofali. Tafadhali njoo uone kile ambacho tumetimiza!

Hapo awali, Crabshack ilikuwa na uwezo wa kuhudumia watu 10 kila siku. Leo, hoteli hii inahudumia wateja kati ya 500 na 1,000 kila siku wakati wa msimu wa wageni wengi, na mapato ya kila mwezi wakati mwingine hufika dola 30,000. Hoteli hiyo imeajiri wafanyakazi 42 kutoka kijiji hicho, baadhi yao wakiwa waanzilishi wa kikundi hicho cha vijana.

Alipoulizwa jinsi Crabshack imesaidia vijana katika kijiji chake, Bw. Mazinga alisema haraka kuwa wafanyakazi huweza kuwapeleka watoto wao shule bila matatizo ya kifedha. Anaeleza kuwa alinufaika kibinafsi, kufikia kile kilichoonekana kutowezekana kwake alipofanya kazi kama mpishi katika hoteli za kifahari.

"Hapo zamani, nilikuwa nikitoka nyumbani saa kumi na moja asubuhi na kurudi nyumbani baada ya saa nne usiku kila siku, na niliishi katika nyumba iliyojengwa kwa udongo. Pia nilihangaika kuwapeleka watoto wangu shule za mitaa. Sasa, ninaishi katika nyumba yangu nzuri iliyojengwa kwa matofali. Tafadhali njoo uone kile ambacho tumetimiza!" anasema kwa furaha Bw. Mazinga, anayemiliki nyumba iliyo umbali wa mita 300 tu kutoka hoteli yake.


Bw. Newton Kanhema ni Naibu Mkurugenzi, Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa - Nairobi.