探花精选

Redirecting...

探花精选

The Africa Renewal website has relocated to:

You are being redirected automatically. If not, click the link above.

COVID-19 inakumbusha jukumu la mabunge katika kuimarisha jamii -Guterres

Get monthly
e-newsletter

COVID-19 inakumbusha jukumu la mabunge katika kuimarisha jamii -Guterres

UN News
30 June 2020
By: 
Katibu Mkuu wa UN Ant贸nio Guterres (katika picha hii ya maktaba) alipohutubia kikao maalum cha Bunge la Italia
UN /Rein Skullerud
Katibu Mkuu wa UN Ant贸nio Guterres (katika picha hii ya maktaba) alipohutubia kikao maalum cha Bunge la Italia

Leo ni siku ya mabunge duniani ambapo Umoja wa Mataifa unasema ni siku muhimu ya kutambua mchango muhimu wa mabunge katika kupaza sauti za wananchi na pia kushawishi uundaji wa sera.

Katika ujumbe wake hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anasema kuwa听鈥渕imi nimewahi kuwa mbunge, na ninaguswa sana na wajibu na heshima ya kuwakilisha wananchi na kukidhi matarajio yao. Mabunge yana jukumu mahsusi katika kusongesha haki za binadamu na kusongesha maendeleo endelevu.鈥

Katibu Mkuu amesema kuwa kuliko wakati wowote ule, hivi sasa katika zama za janga la la virusi vya Corona au COVID-19, jamii inakumbushwa majukumu hayo muhimu.

鈥淜adri dunia inapokabiliana na janga hili, tunaona umuhimu wa kipekee wa uwepo wa mifumo thabiti ya afya, mitandao ya uhakika na bora ya hifadhi ya jamii na ukuaji uchumi wa kutosheleza unaochechemua ajira zenye hadhi,鈥听amesema Katibu Mkuu.

Bwana Guterres ameenda mbali zaidi akisema kuwa,听鈥渢unaona pia wale walio hatarini zadi kwenye jamii zetu kama vile wanawake wakibeba mzigo mkubwa. Ukosefu wa usawa, unyanyapaa, mgawanyiko na utete katika dunia yetu vimeongezeka maradufu mbele ya macho yetu.鈥

Amesema kwa kuzingatia mazingira ya sasa,听鈥渘i lazima tuchukue hatua pamoja kujenga upya, mustakabali wenye usawa zaidi, wenye mnepo na wenye manufaa kwa wote. Nasihi mabunge ya nchi kokote pale kutekeleza kwa kina majukumu yao na kusongesha hatua endelevu na jumuishi.鈥

Katibu Mkuu amesema hilo linapaswa kujumuisha na kuratibiwa pamoja na mashirika ya kiraia, ili kuwa na mipango ya kitaifa dhidi ya ubaguzi wa rangi.

Amesema na wakait huo,听鈥渢ukumbuke kuwa hakuna taifa ambalo linaweza kufanikiwa peke yake. Hebu na tutumie fursa hii kujenga upya mustakabali wetu wa pamoja, tuchukue hatua za kijasiri na kubwa kwa tabianchi na kuweka haki za binadamu听听na utu kuwa kitovu cha kazi yetu.鈥

听Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitia azimio lake namba 听 la tarehe 22 mwezi Mei mwaka 2018, lilipitisha Juni 30 kuwa siku ya mabunge duniani kwa kutambua mchango wa chombo hicho katika mipango na mikakati ya kitaifa katika kuhakikisha uwazi na uwajibikaji katika ngazi za kitaifa na kimataifa.

Tarehe hiyo ya Juni 30 ni tarehe ambapo pia mwaka 1889, chama cha mabunge duniani, IPU kilianzishwa.