探花精选

Redirecting...

探花精选

The Africa Renewal website has relocated to:

You are being redirected automatically. If not, click the link above.

Mfanyakazi yuko njia panda : Afe kwa njaa au virusi? - ILO

Get monthly
e-newsletter

Mfanyakazi yuko njia panda : Afe kwa njaa au virusi? - ILO

UN News
11 May 2020
By: 
Mfanyikazi akifanyakazi katika Kampuni ya Clean World akitoa mabaki ya sabuni inayotoka katika ukanda wa conveyor
ILO Photo/John Isaac
Mfanyikazi akifanyakazi katika Kampuni ya Clean World akitoa mabaki ya sabuni inayotoka katika ukanda wa conveyor

Mikakati ya kutaka watu kubaki majumbani ili kuzuia kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa聽Corona聽au COVID-19 imewaweka wafanyakazi njia panda akiwa hafahamu achague afe njaa na familia yake au afe kwa virusi.

Mikakati ya kutaka watu kubaki majumbani ili kuzuia kuenea聽kwa聽virusi聽vya ugonjwa wa Corona聽au聽COVID-19 inatishia kuongeza聽kwa聽asilimia 56 viwango vya umaskini miongoni mwa wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi walioko nchi za kipato cha chini.

Shirika la kazi聽聽la Umoja wa Mataifa,聽聽limesema hayo katika nyaraka yake mpya wakati huu ambapo mataifa kadhaa yamechukua hatua kali kuzuia watu kutoka majumbani ikiwemo hata kufanya biashara ndogo ndogo kama聽njia聽ya kudhibiti COVID-19.

ILO聽inaesema kiwango hicho cha ongezeko la umaskini聽kwa聽asilimia 56 kati nchi hizo za kipato cha chini ni kikubwa ukilinganisha na asilimia 52 nchi za kipato cha juu na asilimia 21聽kwa聽walioko nchi za kipato cha kati.

Shirika hilo linasema kuwa,聽鈥渢akribani wafanyakazi bilioni 1.6 wa sekta isiyo rasmi kati ya wafanyakazi bilioni 2 wa sekta hiyo duniani kote, wameathiriwa na hatua za kukaa ndani聽au聽kutotembea hovyo. Wengi wao wako kwenye sekta zilizoathiriwa zaidi聽au聽kwenye maeneo ambayo kuna madhara makubwa. Sekta hizo ni pamojana zile za malazi, chakula, uzalishaji, biashara ya jumla na rejareja na zaidi ya wakulima milioni 500 wanaozalisha chakula聽kwa聽ajili ya wakazi wa mijini.鈥

Ripoti inasema kuwa wanawake ndio wamekumbwa zaidi kwenye sekta hizo na kwamba,聽鈥渨akati wafanyakazi wakihitaji kufanya kazi kulisha familia zao, hatua za kudhibiti COVID-19 katka nchi nyingi haziwezi kutekelezwa ipasavyo. Hii inaathiri juhudi za serikali za kulinda jamii na kukabiliana na janga.鈥

Kama hiyo haitoshi,聽ILO聽inasema mvutano huo unaweza kuleta mvurugano katiika nchi ambako sekta isiyo rasmi ni kubwa.

鈥淲afanyakazi wa sekta isiyo rasmi wakiwa hawana mbinu yoyote ya kusaidia familia zao, wanabakia kwenye mkanganyiko, wafe聽kwa聽njaa聽au聽kwa聽virusi,鈥澛聽imesema ripoti hiyo ikiongeza kuwa hali inakuwa mbaya kutokana na kuongezeka聽kwa聽uhaba wa chakula ambao unakumba zaidi wale waliokuwa kwenye sekta isiyo rasmi.

Ikimulika wafanyakaiz wa ndani, ripoti inasema kuwa聽kwa聽wafanyakazi hao milioni 67 ambao asilimia 75 kati yao wako kwenye sekta isiyo rasmi, suala la ukosefu wa ajira limekuwa tishio kama vilivyo聽virusi聽vyenyewe vya Corona.

鈥淲engi wao hajawaweza kufanya kazi, iwe聽kwa聽ombi la waajiri wao聽au聽kwa聽zuio la kudhibiti kuenea聽kwa聽Corona. Wale ambao wanaendelea na ajira, wako hatarini zaidi kuambukizwa Corona wakihudumia familia kwenye makazi binafsi.聽Kwa聽wafanyakazi wa ndani wahamiaji milioni 11 hali ni mbaya zaidi,鈥澛聽imesema ripoti hiyo.

Akizungumzia ripoti hiyo, Philippe Marcadent, Mkuu wa kitengo cha sekta isiyo rasmi,聽ILO聽amesema kuwa,聽鈥淛anga la COVID-19, linaongeza ukosefu wa usawa ambao tayari ulikuwepo. Hatua za kisera lazima zihakikishe msaada unafikia wafanyakazi na kampuni zenye uhitaji zaidi.鈥

Kimaeneo, hatua za kuzuia watu kutochangaman zimekuwa na madhara zaidi huko Amerika ya Kusini ikifuatiwa na nchi za kiarabu, halafu Afrika, kisha Asia na Pasifiki na Ulaya na Asia ya Kati.

ILO聽inapendekeza kuwa nchi zinapaswa kufuata mkakati mchanganyiko unaozingatia athari zote za kiafya na kiuchumi.

Kwa聽mantiki hiyo, nchi zinatakiwa kuwa na sera zinazopunguza fursa za wafanyakazi wa sekta isiyo rasmi kupata maambukizi ya聽virusi, kuhakikisha wale wanaoambukizwa wanapata huduma ya afya, kuwapatia msaada wa kipato na chakula wao na familia zao pamoja na kuzuia hali ya sasa isilete madhara ya kudumu ya kiuchumi.